
CROSAT YATEMBELEA TARI NA KUKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO
June 11, 2025
CROSAT AND TAHA TO SHAPE THE FUTURE OF TANZANIAN AGRICULTURE
June 23, 2025Viongozi wa Jumuiya ya Wanasayansi wa Kilimo Mazao (CROSAT) wakiongozwa na Katibu Mkuu, Ndugu Patrick Ngwediagi wamemtembelea Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ofisini kwake jijini Dodoma na kufanya mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hiyo na Wizara ya Kilimo.
Kupitia kikao hicho, CROSAT ilishukuru Wizara yake kwa ushirikiano iliyopata tangu kuanzishwa kwake pamoja na kuomba kuimarisha ushirikiano zaidi katika utekelezaji wa mipango ya Chama icho na kushirikishwa katika mipango ya uendelezaji wa sekta ya kilimo.
Katika mazungumzo hayo Mhe. Hussein Bashe aliahidi kuishirikisha CROSAT katika mipango ya uendelezaji wa sekta ya kilimo.
Sambamba na hilo viongozi wa CROSAT walikutana na Naibu Katibu Mkuu (Ushirika na Umwagiliaji) Dkt. Stephen Nindi pamoja na Kaimu mkuu wa Idara ya Maendeleo na Mazao, Ndugu. Upendo Mndeme na kuzungumza mambo mbalimbali ili kuimarisha ushirikiano.

Viongozi wa CROSAT, Katibu mkuu (kushoto), Rais (kati) na Naibu Katibu Mkuu wizara ya Kilimo (kulia) wakifurahia jambo






