
CROSAT Enhances Collaboration with Zanzibar Agricultural Research Institute (ZARI)
April 3, 2025Viongozi wa Jumuiya ya Wanasayansi wa Kilimo Mazao (CROSAT) wakiongozwa na Katibu Mkuu, Ndugu Patrick Ngwediagi wametembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) na kufanya mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za Makao Makuu ya TARI zilizopo mkoani Dodoma.
Katika mazungumzo hayo ujumbe wa CROSAT uliitambulisha rasmi CROSAT, kushukuru kwa ushirikiano ambao TARI imekuwa ikionyesha kwa CROSAT pamoja na kubainisha maeneo ambayo taasisi hizi zinaweza kushirikiana.
Aidha, katika mazungumzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dr. Deusdedith Mbanzibwa ambaye aliongoza maafisa wengine wa TARI alipongeza juhudi za CROSAT kuwaweka pamoja wadau wa kilimo mazao na ameahidi kuwa TARI itaendelea kushirikiana na CROSAT kwa karibu zaidi.
Uongozi wa TARI uliahidi kushirikiana na CROSAT katika uandishi wa miradi na pia kuialika kwenye matukio muhimu ikiwemo mikutano ya IPR ambapo itapewa nafasi ya kuwasilisha mada.