
CROSAT Elects New Leadership Team for 2026–2028 Tenure
December 30, 2025Wanachama wa CROSAT, wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Mahinda Athuman, wameshiriki kikamilifu TARI Marathon iliyofanyika tar. 2 Agasti 2026, mkoani Dodoma.
Marathoni hii ni sehemu ya shughuli za kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI). Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (MB).
Kwa CROSAT, ushiriki huu ni uthibitisho wa dhamira yake ya kuunga mkono utafiti na kuchangia maendeleo ya kilimo nchini. Pia ni hatua nyingine ya kuimarisha uhusiano wake na TARI ili kuweza kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya kilimo nchini.
Aidha, CROSAT inawakaribisha wananchi kwenye Banda la CROSAT katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea kufanyika mkoani Dodoma, viunga vya Nzuguni; kujifunza mambo mbalimbali, kazi inayozifanya na utaratibu wa kujiunga na Chama.
#CROSAT #TARIMarathon #Miaka10TARI #Kilimo #Utafiti #Dodoma







